Changamoto ya Usafiri yatafutiwa ufumbuzi.
Mkurugenzi mkuu na CEO wa Luba Express, Luba Fishing Materials Shop na Luba Video Shooting, Mhe: NDIHOKUBWAYO Salutier, amesema wakati huu ambapo serkali bado inapambana na maambuki ya virusi vya Corona hakuna budi Abiria wetu kuwa na Subra kuhusiana na huduma za usafirishaji wa kutoka nchini Burundi kuelekea Nchini Tanzania ambazo zilikuwa zikitolewa na Shirika la Luba Express, na hivyo kutoa wito kuwa changamoto hiyo ya kukosa usafiri wa kwenda nje ya nchi itatatuliwa hivi karibuni maana shirika hilo linaendelea kufanya mazungumzo na Serkali ili kuona kama inaweza kutoa Ruksa ya kuendelea na huduma zake za usafirishaji nje ya Nchi.
