ABIRIA WA LUBA EXPRESS KWENYE LEVEL SEAT
Moja kati ya vitu vilivyo wafurahisha abiria wa Luba Express ni mpango wake wa Level Seat yaani Watu kusafiri bila kubanana na hilo limeanza baada ya Uongozi wa Luba Express kuongeza idadi ya Magari yanayo safiri kutoka Bujumbura kuelekea Mpakani mwa Tanzania na hivyo kupunguza ule msongamano wa Abiria katika Gari. Hayo yamezungumzwa na Mmoja wa Abiria wakati walipokuwa wamewasili katika kituo cha Luba Express Mjini Rumonge.





